1 Corinthians 9:1-2

Haki Za Mtume

1 aJe, mimi si huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Isa, Bwana wetu? Je, ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana? 2 bHata kama mimi si mtume kwa wengine, hakika mimi ni mtume kwenu, kwa maana ninyi ni mhuri wa utume wangu katika Bwana.

Copyright information for SwhKC